Kama Wewe ni Mwanamke Unayetaka Kumvutia Mume Wako, Jipambe Hivi

Rafiki yangu mpendwa katika Kristo,

Wanawake wa siku hivi wamekuwa wakihangaika kutafuta kila namna ya kuwavutia waume zao. Njia mojawapo ambayo wamekuwa wakiitumia ni kujipamba kwa namna mbalimbali. Lakini pamoja na kujiamba huko, baadhi bado hawawavutii kabisa waume zao.

Kama wewe ni mmojawapo wa wanawake hao, bila shaka umewahi kujiuliza “hivi ninakwama wapi”? Kama hujawapi kupata jibu la swali hilo, basi fuatana nami, katika makala ya leo ili nikushirikishe ni wapi unakwama na ufanye nini ili umvutie mume wako.

Katika Biblia, mavazi ni mojawapo ya mada ambayo imewekewa maelezo bainifu na Mungu. Kwa mfano, katika agano jipya, kuna sehemu mbili ambazo zimetoa melekezo yanayofanana kuhusu mavazi japo kwa muktadha tofauti.

Sehemu hizo ni Waraka wa kwanza wa Mtume Paulo kwa Timotheo (1 Timotheo 2: 9-10) na Waraka wa kwanza wa Mtume Petro kwa watu wote (1 Petro 3:3-4). Sehemu zote hizi zinatoa maelekezo mahususi juu ya namna wanawake wanavyapaswa kujipamba.

Wakati muktadha wa Mtume Paulo ni  ni mwenendo wa wanawake wakiwa kanisani, muktadha wa mafundisho ya Petro yanahusiana na mwenendo wa mwanamke akiwa nyumbani. Hata hivyo, kuna mfanano mkubwa katika mafungu haya juu ya kanuni zinazoelezwa ndani yake.  

Katika makala ya leo, tutachambua kwa kifupi mafundisho ya Petro kuhusiana na namna mwanamke anavyopaswa kujipamba akiwa nyumbai ili kumvutia mume wake.

Soma : Je, unataka kujua kwa nini watu hupenda kuvaa ‘vimini’? Bonyeza hapa.

Neno la Mungu linasema“Kadhalika ninyi wake, watiini waume zenu; kusudi, ikiwa wako wasioliamini Neno, wavutwe kwa mwenendo wa wake zao, pasipo lile Neno; wakiutazama mwenendo wenu safi, na wa hofu. Kujipamba kwenu, kusiwe kujipamba kwa nje, yaani, kusuka nywele; na kujitia dhahabu, na kuvalia mavazi;  bali kuwe utu wa moyoni usioonekana, katika mapambo yasiyoharibika; yaani, roho ya upole na utulivu, iliyo ya thamani kuu mbele za Mungu. Maana hivyo ndivyo walivyojipamba wanawake watakatifu wa zamani, waliomtumaini Mungu, na kuwatii waume zao” (1 Petro 3:3 – 5).

Katika mafungu haya, kimsingi Petro anaeleza kitu kile kile kilichoelezwa na Paulo katika 2 Timotheo 2:9-10. Hata hivyo, Petro anaongezea mambo mawili kwa wanawake ambayo ni muhimu katika kuimarisha uhusiano mzuri na waume zao na kuwaleta kwa Kristo kwa wale ambao si wakristo.

Jambo la kwanza analoongezea Mtume Petro hapa,  ni utii kwa waume zao na la pili ni roho ya upole na utulivu. Utii huu unaoweza kuwaleta waume zao kwa Kristo hauletwi na mwonekano mzuri wa nje (mavazi au mapambo ya bei mbaya) bali unatokana na roho ya upole na utulivu.

Kama nilivyodokeza awali, muktadha wa mafundisho ya Paulo (2 Timotheo 2:9-10) ni katika ibada kanisani wakati muktadha wa mafundisho ya Petro ni nyumbani. Kufanana kwa mafundisho ya Paulo na Petro wakati yalitolewa katika muktadha tofauti ni ishara kwamba kanuni zinazohusu mwonekano wa mkristo zinatumika katika sehemu mbalimbali za maisha ya mwanadamu.

Vitu vilivyokatazwa mahali fulani haviwezi kukubalika mahali pengine. Kwa mfano, kama vimini havikubaliki kanisani, haziwezi pia kukubalika nyumbani. Yaani, vimini havikubaliki kanisani na nyumbani pia.

Petro anatoo mwongoz mzuri kwa baadhi ya  wanawake wanaodhani kuwa wanaweza kuwavutia waume zao kupitia mwonekano wa nje na hivyo wanatumia muda mwingi na fedha nyingi kujipamba na kuvalia mavazi wanayodhani yatawavuta wanaume.

Kupitia mafundisho ya Petro, kumbe njia bora ya kuwavuta wanaume ni kuwatii. Kwa kufanya hivyo, wanawake wataimarisha uhusiano wao na waume zao na pia wanaume wasio wakristo, wanaweza kuvutwa na mwenendo wa wake zao na kuamua kumwanini Kristo.

Kwa wanawake wanaodhani wanaweza kuwavuta wanaume kwa kujipamba kwa nje, Petro anawaonya kuwa hiyo siyo njia sahihi na anawaelekeza kuwa wasihangaike na kujipamba kwa nje bali wahangaike na  utu wao wa ndaniusioonekana, katika mapambo yasiyoharibika; yaani, roho ya upole na utulivu, iliyo ya thamani kuu mbele za Mungu.

Maelekezo haya ya Petro  yanafanana na maelekezo ya Paulo katika 1 Timotheo 2:9-10. Badala ya kuhangaika na kutafuta mvuto wa nje, Petro anawaelekeza wanawake watafute kujipamba kwa ndani kwa kumkaribisha Yesu akae ndani ya mioyo yao ili abadilishe utu wao wa ndani usioonekana ili hatimaye utu huo uonekane katika matendo mema ambayo ni pamoja na roho ya upole na utulivu. Bila shaka mwanamke mwenye roho ya upole na utulivu atakuwa na utii kwa mume wake.

Ni vizuri ifahamike kuwa Petro hamaanishi kuwa wanawake waache kabisa kujiweka vizuri katika mwonekano wao wa nje. La hasha. Wanawake wanapaswa kuwa na mwonekano mzuri wa nje unaomtukuza Mungu lakini mwonekano huu hautakuwa na maana yoyote ikiwa watakuwa hawana utu wa moyoni unaoleta utii na roho ya upole na utulivu.

Kwa hiyo, mwanamke anayetaka kumvutia mume wake anapaswa kuwa na mwonekano mzuri wa nje unaomtukuza Mungu pamoja na kuwa na utu wa ndani ambao utamfanya kuwa mtiifu kwa mume wake na kuwa na roho ya upole na utulivu. Kwa kufanya hivyo, wanawake watakuwa wamefuata mfano wa wanawake wa zamani ambao walijipamba kwa ndani na matokeo yake walikuwa ni wanawake wanaomtumaini Mungu na kuwatii waume wao.

Je, unataka kujifunza zaidi kuhusu mada hii?

Basi jipatie kitabu chetu kinachoitwa Mwonekano wa Mkristo: Kanuni Zinazokubalika Kibiblia, Kiafya na Kijamii Kuhusu Mavazi, Mapambo na Vipodozi. Ili kupata kitabu hiki, bonyeza hapa.

Je, unataka kujifunza zaidi kuhusu mapngo wa Mungu kuhusu mafanikio yako?

Basi jiunge na mtandao wa Mkristo na Maisha ya Mafanikio. Mtandao huu umeanzishwa kwa kusudi la kuwapatia maarifa ya msingi katika nyanja mbalimbali za maisha. Katika mtandao huu utapata maarifa katika maeneo ya fedha, biashara, uwekezaji, mahusiano, malezi ya watoto na mambo mengine ya kiroho kupitia email yako kila zinapowekwa kwenye mtandao huu.

Kujiunga na mtandao huu, jaza fomu hii hapa chini.

About Devotha Shimbe

Devotha Shimbe ni Mwalimu na mwanasaikolojia. Amepata pia mafunzo ya Theolojia. Devotha amejitoa kumtumikia Mungu katika maisha yake yote na amekuwa akifundisha na kutoa semina mbalimbali kuhusu mahusiano na maisha ya kiroho kwa ujumla.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *