Rafiki yangu mpendwa, Mimi siyo mfuatiliaji kabisa wa vyombo vya habari. Lakini siku ya leo nimejikuta nasikiliza matangazo ya kituo kimoja cha radio wakati napata chakula katika mgahawa fulani. Kila baada ya muda kulikuwa na matangazo ya biashara yanayohamasisha wasikilizaji kubeti ili kubashiri matokeo ya mechi za mashindano ya kombe la dunia yanayoendelea huko Qatar.…