KUHUSU WAANDISHI

Huduma hii ya Mkristo Na Maisha Ya Mafanikio inaendeshwa na Simeon Shimbe na Devotha Shimbe ambao ni mume na mke waliojitoa kuwasaidia wengine kufikia mafanikio makubwa kiuchumi, kiroho na kimahusiano.

KUHUSU SIMEON SHIMBE

Simeon Shimbe ni mchumi kitaaluma, mwandishi wa vitabu na makala na mjasiriamali. Amekuwa akiandika kuhusu masuala ya fedha, biashara na uwekezaji na masuala mbalimbali ya kiroho.

KUHUSU DEVOTHA SHIMBE

Devotha Shimbe ni Mwalimu na mwanasaikolojia. Amepata pia mafunzo ya Theolojia. Devotha amejitoa kumtumikia Mungu katika maisha yake yote na amekuwa akifundisha na kutoa semina mbalimbali kuhusu mambo ya kiroho na maisha kwa ujumla hususani juu ya mahusiano (uchumba na maisha ya ndoa), mwenendo wa mkristo, malezi ya watoto na vijana, elimu ya kikristo na kadhalika.