KITABU: HOMILIA KWA WALEI

HOMILIA KWA WALEI: USTADI WA KUANDAA NA KUWASILISHA MAHUBIRI

Kitabu hiki kinaeleza, hatua kwa hatua, kanuni na mbinu rahisi za kuandaa na kutoa mahubiri yenye mguso kwa hadhira. Kwa kusoma kitabu hiki, wale wanaopata taabu wanapotakiwa kuhubiri, wataweza kujifunza mbinu na kanuni hizi na kuwa wahubiri wazuri. Kwa kuwa kuhubiri ni wajibu wa kila muumini, kitabu kinamlenga kila muumini. Hata wale ambao wana kipaji cha kuhubiri na wamekuwa wakihubiri, bado wanahitaji kujifunza zaidi ili kuboresha uwezo wao. Hivyo, kitabu hiki kitawafaa wao pia.

Kitabu kimeandikwa kwa namna ambayo ni rahisi kueleweka na kina mambo muhimu tu ya kufanyia kazi na hakijaingia kwa undani katika nadharia nyingi za kihomilia zisizohitajika ili waweze kujisomea wao wenyewe na kuelewa.

Kwa kusoma kitabu hiki utaweza kupata maarifa mengi, yakiwemo yafuatayo

  • Aina mbalimbali za mahubiri
  • Hatua kumi za uandaaji wa hubiri
  • Namna ya kujifunza Biblia ili uweze kuandaa hubiri
  • Mambo ya kuzingatia katika kuchagua mada ya hubiri, wazo kuu na kichwa cha hubiri
  • Sehemu kuu tatu za hubiri na namna ya kuziandaa : Utangulizi, kiini na hitimisho
  • Namna ya kuwateka watu wasichoke kusikiliza hubiri lako  na wasilisahau baadaye
  • Urefu wa hubiri : Hubiri linapaswa kuchukua muda gani?
  • Jinsi ya kujenga kujiamini na kushinda hofu wakati wa kuwasilisha hubiri
  • Mwonekano wa mhubiri (mavazi, mapambo na vipodozi)
  • Matumizi sahihi ya sauti na kipaza sauti
  • Matumizi sahihi ya viungo vya mwili wakati unahubiri
  • Mambo ambayo hupaswi kutamka au kufanya wakati wa hubiri
  • Kuhubiri kupitia mkalimani
  • Namna unavyoweza kufanya tathmini ya hubiri lako

Namna ya kitabu hiki Ili uweze kuelekezwa namna ya kupata kitabu hiki, wasiliana nasi kupitia namba za simu; +255754-405582 (Simeon Shimbe), +255714-606278 (Devotha Shimbe) na E-mail: spshimbe@gmail.com, devothashimbe@gmail.com