USTADI WA KUFUNDISHA NA KUHUBIRI WATOTO
Kitabu hiki kina maarifa ya msingi yanayohitajika kwa ajili ya kuhubiri na kuwafundisha watoto elimu ya kiroho katika karne ya 21. Kutokana na maendeleo ya Sayansi ya teknolojia, ufundishaji wa siku hizi ni tofauti kabisa na wa zamani. Kwa kuzingatia ukweli huo, mbinu za kufundisha na kuhubiri zilizoelezwa katika kitabu hiki ni za kisasa kabisa zinazolenga kukidhi mahitaji ya kujifunza ya watoto wa siku hizi.
Kitabu hiki kinalenga kuwasaidia wazazi, walezi, walimu wa dini na wahubiri wa watoto ili waweze kupata ustadi wa kufundisha na kuhubiri watoto kwa ufanisi. Hivyo, hiki ni kitabu kwa watu wote wanaohitaji maarifa ya msingi kwa ajili ya kufundisha na kuhubiri watoto nyumbani, shuleni na kanisani. Japo, kimeandikwa kikilenga mazingira ya kanisani, lakini maarifa yaliyomo yanafaa kutumika pia katika mazingira ya nyumbani na shuleni.
Kitabu hiki kina mambo mengi ya kujifunza. Baadhi ya mambo utakayojifunza kwa kusoma kitabu hiki ni pamoja na yafuatayo:
- Tofauti ya watoto wa siku hizi na wa zamani
- Tofauti ya ufundishaji wa siku hizi na wa zamani
- Namna ya kujiandaa kufundisha au kuhubiri na kuandaa mazingira ya kujifunzia na kuhubiri watoto
- Kuwaelewa watoto na umri mbalimbali na hali za ukuaji wao kimwili, kiakili, kiroho na kijamii
- Kufundisha na kuhubiri watoto wenye mahitaji maalum
- Matumizi ya visa na hadithi katika kufundisha na kuhubiri watoto wa umri mbalimbali
- Kufundisha nyimbo na muziki kwa watoto wa umri mbalimbali
- Kuwafundisha watoto kuomba
- Namna ya kuwafundisha watoto kutumia Biblia
- Namna unavyoweza kufundisha na kuhubiri watoto kupitia sanaa, michezo na kazi za mikono
- Namna unavyoweza kudhibiti nidhamu ya watoto wa umri mbalimbali
- Ustadi wa kuwasiliana na watoto
- Namna unavyoweza kuwasaidia watoto kukua kiroho na kuwaandaa kwa ajili ya ufalme wa Mungu
Jinsi ya kupata kitabu hiki
Ili uweze kuelekezwa namna ya kupata kitabu hiki, wasiliana nasi kupitia namba za simu; +255754-405582 (Simeon Shimbe), +255714-606278 (Devotha Shimbe) na E-mail: spshimbe@gmail.com, devothashimbe@gmail.com